Nakubalika zaidi nchi za nje kuliko Nyumbani Nigeria - Iyanya

Msanii wa Nigeria Iyanya Mbuk amesema anakubalika zaidi nchi za nje zaidi ya anavyokubalika nyumbani kwao Nigeria.


Iyanya anayesumbua Afrika kwa sasa na na hit yake ‘Kukere’, amezungumza hayo katika mahojiano na gazeti la PUNCH.

“Sikubaliki Nigeria kama ninavyokubalika nchi za nje. Nadhani hayo ni malipo ambayo ‘Kukere’ imeniletea katika kipindi kifupi. Ukweli ni kwamba nilikuja na Kukere kutengeneza pesa kwasababu Wanaijeria walikuwa hawasikilizi muziki wa RnB. Ona wapi imenifikisha leo”. Alisema Iyanya.

Hli ni Moja kati  ya magari ya Iyanya

Iyanya ambaye alikuja Tanzania katika Fiesta ya Dar es salaam mwaka huu, pia amekanusha maneno yanayosemwa kuwa wasanii wengi wanatabia ya kujionesha kwenye mitandao ya kijamii. Iyanya ameongeza kuwa haoni sababu ya kuficha kile ambacho Mungu amemuwezesha kupata kwa kuzingatia kuwa ni mafanikio yake.

“I mean if God has blessed me, there is no reason to hide that. We are not showing off. After all, everyone knows Iyanya’s story. Whenever I post pictures of my cars or money on Instragram, the public should understand that it is just my own way of saying if God can do it for me, He can for you too.”

Magari ya Iyanya

Hivi karibuni msanii huyo aliingia deal za endorsement na makampuni mbalimbali Nigeria yakiwemo MTN, Zinox Computers na Solo Phones.



Iyanya pia alikanusha uvumi kuwa hivi karibuni alinunua magari manne kwa siku moja na kusema alinunua gari moja jipya na kuweka picha yake Instagram, na jumla kwa sasa anamiliki magari manne.




Previous Post Next Post