VIDEO: EBSS YATANMGAZA MKAKATI MPYA WA MATUMIZI YA ZAWADI YA MSHINDI,NI BAADA YA NEY WA MITEGO KUTOA HIT SONG YA NASEMA NAO"

Mkurugenzi wa Benchmark Productions, Rita Paulsen amesema mshindi wa mwaka huu wa Bongo Star Search atasaini mkataba maalum na BSS wa namna fedha atakazoshinda zitakavyotumika kwa makusudi maalum ya kumsaidia kimuziki.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Madam Rita amesema kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kuwa washindi wa BSS hawafiki popote licha kushinda fedha nyingi ambazo amesema wao huzitumia kwa matumizi mengine tofauti na muziki kama inavyotakiwa.

“Kutokana na changamoto za watu kusema kwamba washiriki hawatoki. Tumegundua kwamba mtu akipewa hela, hela anazopewa kwa kawaida anatakiwa azitumie pia kujijenga kimuziki. Lakini labda kutokana na maisha au nini, tumegundua kwamba wasanii hawawezi kutumia hizo hela kujijenga. Wanaweza kutumia kwa vitu vingi ambavyo ni mahitaji pia sijui nyumba, gari. So tumeamua mshindi anasaini contract na Management Company. Kwahiyo hela yake na management company, yeye mwenye anatoa hela yake, management company inaleta proposal, tunatengeneza video kadhaa, tunatengeneza promotion ya wimbo wako. Kutakuwa na mwanasheria na yeye mwenyewe anaauthorise ile hela inaenda kufanya hivyo vitu. Kwahiyo tumeona kama 20 percent ya hela atakazozipata itabidi zimtengenezee yeye future,” alisema.


Washiriki watano waliongia fainali ambao ni  Elizabeth Mwakijambile,Melissa John,Maina Thadei,Amina Chibaba na Emmanuel Msuya
Fainali ya shindano hilo itafanyika Jumamosi hii, Escape 1 jijini Dar es Salaam ambapo wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Barnaba,Shaa,Snura,Makomando,Borabora Band pamoja na mshini wa mwaka jana Walter Chilambo


Barnaba akiongea na waandishi wa habari
Makomando nao wakionyesha Staili yao mpya, Umeniroga watakayoitambulisha siku fainali
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA