HOT NEWS: BIFU YA ADAMU JUMA NA NISHER

Nani anakumbuka video ya ice cream ya noorah ? hii ndio video iliyomtambulisha adam juma na visual lab kipindi hicho haijaenda next level. adam juma ni nguli katika utengenezaji wa video na mhimili mkubwa ambao sidhani kuna mtu anaweza kuja kuchukua nafasi yake. ametengeeza mamia ya video za bongo kuanzai icecream , baridi kali ya enika , mwana fa na lady jaydee hawajui , kuja kwa md dogg.kusema kweli hauwezi kumaliza list ya video ambazo adam juma amefanya.




baada ya utawala wake kwa miaka yote hii ilipofika mwaka jana kuna “chalii” mmoja wa arusha alianza naye kufanya videos.jamaa anajulikana kama nisher. mshkaji alianza kufanya video fulani hivi za maunderground na kama wewe sio mfuatiliaji mzuri wa videos za bongo unaweza kufikiri kwamba video ya kwanza nsher kuifanya ikawa ni sijutii ya joh makini au listen ya belle 9 , lakini siyo kweli. nisher alikua na video zake nyingine ambazo zilikua hewani.

Baada ya nisher kukubalika sana na watu kwa kufanya video nzuri watu wengi walianza kumpa sifa za kutosha na wengine kudiriki kumvua ufalme wa video adam juma kitu ambacho kilizua utata. miezi saba iliyopita adam juma aliamua kuvunja ukimya na kutupia comments zake kwa youtube katika video ya mama yeyoo ya G.nako feat ben pol aliyoifanya nisher. adam juma alimponda nisher kwa kutumia filters na effects .

adam-juma-youtube-comment

kwa sasa adam juma ameacha kutengeneza music videos lakini jambo la kushangaza ni picha aliyoipost nisher kwenye account zake za twitter,facebook na instagram akiiponda kimafumbo kampuni ya visual lab next level. nisher aliupload picha yenye maneno”i’m not next level, i’m a new game”.



kitendo hiki kilimkasirisha adam juma na kufanya naye atoe yaliyo moyoni kuhusu picha hii ya nisher. adam juma alizidi kumponda nisher kutokana na kitendo hicho.
adam instagram
Previous Post Next Post