Rapper Kala Jeremiah Apata Shavu La Kuwa Balozi wa Pepsi



Rapper wa Dear God, Kala Jeremiah ameingia mkataba na kampuni ya Pepsi kama balozi wake mpya. Ameiambia Bongo5 kuwa mkataba huo ni wa miezi sita.





Kala Jeremiah baada ya kusaini mkataba

“Kwangu mimi ni furaha kwasababu kama kazi zangu zimetambulika kiasi hicho na kukubalika kuwa balozi wa kampuni kubwa kama hiyo, nadhani ni kuonesha jinsi gani jamii inakuheshimu na kuthamini kile unachofanya,” amesema Kala.

“Ni hatua kubwa na jinsi gani sasa muziki wetu wa Hiphop unaeleweka vizuri. Kama hip hop inaweza kushawishi makampuni kama hayo kuwekeza nadhani inaeleweka.”

Kala amesema wasanii wa hip hop waendelea kufanya muziki wao kwa akili ili kushawishi watu wengi zaidi. Msikilize hapo chini.



https://soundcloud.com/mdau-halisi/kala-akiongelea-mkataba-wa
Previous Post Next Post