Picha: Jay-Z na Timbaland wakiwa kwenye treni na kujichanganya na watu wa kawaida London na Kuwaacha Fans wakipagawa



Ukiwa super star Mkubwa Duniani watu Huwaga wanataraji kuwaona live mara chache sana wasanii wao wanaowapenda ndio maana ata shoo Msanii akitangaza shoo , asilimia kubwa ya fans watatamani kwenda kumuona live msanii husika ambaye wamekuwa wakimskia na kuona video zake tu pasipo kumuona live .

 Hii imekuwa tofauti kwa Jay Z kwani amewapa ‘surprise’mashabiki wake wa nchini Uingereza baada ya kusafiri kwa treni jijini London kwenda kwenye show yake kwenye uwanja O2 Arena.




Akiwa kwenye treni, Jay Z aliungana na msanii wa kundi la Coldplay, Chris Martin na producer Timbaland, ambaye anamsaidia kwenye ziara yake ya dunia Magna Carta. Martin, ambaye ni rafiki mkubwa wa Jay Z, baadaye aliungana naye jukwaani.





Shabiki aitwaye Jamie Robb alitweet picha baada ya kukutana na Jay kweny treni na kuandika, “What a riot… Just met Jay Z on the tube in London.”

Alieleza pia kuwa Jay Z alikuwa ameongoza na watu kama 10 hivi.

“Coming off the tube and I see Jay Z casually walking up the next escalator next to me… EVERYONE GOES NUTS,” alitweet shabiki mwingine.

Rihanna pia aliwahi kutumia usafiri huo alipokuwa na show nchini Uingereza.
Previous Post Next Post

Popular Items