BEN POL AIMISS M-LAB STUDIO


Ben Pol amezielezea faida na hasara za kuondoka kwenye label iliyomtambulisha, MLab huku akisema kwa sasa hana uhuru wa kurekodi nyimbo nyingi kwa wiki kama alivyokuwa kwenye label hiyo.


“Sasa hivi sina freedom ya kurekodi nyimbo 3 kwa wiki kwasababu itabidi upige simu, ufanye booking hata two weeks before, uende utengeneze beat, unaweza ukarekodi wimbo mmoja miezi miwili au mwezi mmoja. Lakini kipindi nipo MLab unarekodi nyimbo nne, hizi Maneno, Nikikupata, Maumivu, ndani ya wiki moja nimerekodi nyimbo tatu kwasababu una all access ya studio, unaweza ukarekodi hata nyimbo mbili siku moja, yaani hiyo access ndio nimeimiss sasa hivi,” alisema Ben Pol.

Akizungumzia faida za kuondoka MLab, Ben Pol amesema kwa sasa ana meneja wake binafsi ambaye ni kaka yake na hivyo mazingira ya kufanya kazi ni rahisi tofauti na kuwa chini ya uongozi wa label.

“Kunakuwa na mlolongo mkubwa hata kama ikitokea kazi kuona maslahi yake ni adimu sana tofauti na ukiwa unafanya mwenyewe.”


Msikilize zaidi hapa.

https://soundcloud.com/mdau-halisi/ben-pol-kuhusu-kuondoka-mlab-2
Previous Post Next Post