Queen Latifah Amefunguka Kuhusu Rappers Wa Kike Wa Kizazi Hiki Na Kazi Yake Mpya.




Old Skul rapper Queen Latifah amefunguka hivi karibuni kuhusu maisha ya muziki wake na kusema mpango wake mkubwa umewezeshwa zaidi na msaada kutoka kwa Will Smith na Jada Pinkett ambao walimsaidia kuanzisha kipindi chake cha television 'The Queen Latifah Show'. Kipindi chake kinaanza hivi karibu kwenye cable tv CBS huko Marekani na kitazungumzia maisha ya watu tofauti na mambo yao ya maendeleo.


Kuhusu muziki Queen amefunguka kuwa mpaka sasa hakuna MC Au Rapper wa kike aliyeweza kufunika uwezo wa Lil Kim, Missy Elliott,na Foxy Brown. Queen anaamini kuna wasanii wengi wakike ambao wana vipaji ila hawapewi nafasi ya kufanya vizuri, Nicki Minaj anafanya vizuri ila bado hajafika level za wasanii wa zamani Alisema Latifah.

Queen Latifah hajatoa album toka mwaka 2009.

Previous Post Next Post

Popular Items