Kati ya washiriki 130 wa Miss World 2013, 33 pekee waliingia kwenye nusu fainali ya shindano la vazi la ufukweni. Kwa bahati mbaya Miss Tanzania, Brigitte Alfred hakufanikiwa pia kusonga mbele kwenye mchuano huo.
Washiriki wa Miss World 2013 ambalo mwaka huu linafanyika nchini Indonesia, watachuana kwenye mashindano mengine kama kama Top Model, Sports and Fitness, Beauty with a Purpose, Talent Competition na World Fashion Designer Award, kabla ya fainali zenyewe tarehe 28, September.
Washindi wa mashindano mengine nao watatangazwa siku hiyo.
Washiriki walioingia kwenye fainali ya Beach Fashion ni
France, Marine Lorphelin
Indonesia, Vania Larissa
Spain, Elena Ibarbia
Italy, Sarah Baderna
Moldova, Valeriya Tsurkan
Ukraine, Anna Zayachkivska
Philippines, Megan Young
Brazil, Sancler Konzen
China PR – Wei Yu
Jamaica, Gina Hargitay
Ghana, Carranzar Shooter