
Meli yenye usajili wa TANZANIA yakamatwa kwenye ukanda wa SICILY na mamlaka ya askari wa ITALY wakati ikiwa inasafirisha madawa ya kulevya, wasafirishaji hawa walijaribu kuichoma MELI hiyo moto kwa ajili ya kupoteza ushahidi lakini moto huwa uliwaiwa kuzimwa na kikosi maalumu cha zima moto wa majini, Meli hio ilikadiriwa kubeba madawa yenye thamani ya Paundi Million 50, Huku baadhi ya watu waliokua wakihusika tisa(9) wa usafirishaji wa madawa hayo ambao walikua ndani ya MELI hio walijaribu kutoroka kwa kuruka kwenye baharini, lakini zoezi lao hilo lilishindwa kufanikikwa kwa sababu walikua mbali na Nchi kavu na hivo iliwalazimu kuokolewa na kikosi hicho cha Polisi amabao walikua wakiifwatilia MELI hio.

Mzigo huo wa madawa na MELI hio viliokolewa na kupelekwa nchi kavu salama pamoja na watuhumiwa hao ambao kwa sasa wanasubiriwa kuhojiwa kisheria kuhusu usafirishaji huo wa madawa ya kulevya.
Tags:
Social