Kama Ulikuwa Aufahamu: Ndoa ya mtoto wa Bilionea Aga Khan Ilivunjika




Mtoto wa tajiri maarufu hapa duniani Aga Khan amevunja ndoa yake na mwanamama wa Kimarekani ambaye amenunua jumba kubwa la kifahari huko Manhattan lenye thamani ya dola za kimarekani 2.2millioni tayari kuanza maisha yake mapya.
Taarifa hizo zinakuja wakati zikiwa zimepita siku chache tangu mtoto mkubwa wa Aga Khan, Prince Rahim kufunga ndoa na Mwanamama maarufu wa Kimarekani na mrembo Kendra Spears. 


Utajiri wa Aga Khan unakadiriwa kufikia au kupita dola za kimarekani 9billioni lakini haijafahamika rasmi kwamba mtoto wa Aga Khan amepata nini baada ya ndoa kuvunjika. Taarifa zaidi zinasema kwamba wawili hao walikutana wakati wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Columbia.
Mke wa mtoto huyo wa billionea Aga Khan alithibitisha kuvunjika kwa ndoa yao baada ya kununua nyumba ya kifahari maeneo ya Manhattan ili kuanza maisha mapya. 


Prince Khaliya Khan, 36, alinunua jumba hilo la kifahari kwa jina la mtalaka wake, Kristin White, kabla ya wiki kadhaa ya ndoa ya mtoto mkubwa wa billionea Aga khan kwa mrembo na mwanamitindo Kendra Spears.      

Previous Post Next Post