Stori nzima ya kilichotokea mpaka Aunty Ezekiel Kupigwa chupa Club bilicanas hii hapa





Jumapili iliyopita katika ukumbi wa bilicanas mwanadada, Aunty Ezekiel alipigwa chupa na kujeruhiwa vibaya na mwanadada aliyetambuliwa kwa jina la Ivony Bigirwa katika show ya muziki ambapo wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliopo chini ya kampuni  ya Wema Sepetu ya Endless fame walikuwa wakitambulisha nyimbo zao mpya




Chanzo nini?
Baada ya kufuatilia kwa karibu na kuichunguza habari hii bongomovies tumegundua kuwa chanzo kilikuwa ni ‘beef’ la kugombania mwanaume ambaye anasadikika ni mume wa mtu kati ya mwanadada huyo (Ivony) na Aunty Ezekiel



Ilikuaje?
Mpashaji wa habari hii anasema kuwa wanadada hao walikuwa ukumbini hapo na ghafla mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Sunday alitokea ukumbini hapo na ndipo patashika hilo likazuka kila mmoja akidai kuwa jamaa huyo ni wa kwake.
Baada ya vuta nikuvute ndipo uzalendo ukamshinda mwanadada ivony na kuanza kuzichapa na Aunty kabla ya kuamua kuchukua chupa na kumpiga nayo na kumjeruhi maeneo ya mkononi





Hali ya Aunty Ezekiel
Kwa sasa hali yam dada huyu iko vizuri na mpaka tunavyoripoti sasa, habari zinasema amesharuhusiwa kutoka hospitalini kwenda kupumzika nyumbani

News via: BongoMovies
Previous Post Next Post