Hii ndio kauli aliyoitoa January makamba kuhusu bongo movies; Soma na utupe maoni yako





Leo kupitia ukurasa wake wa twitter,  mbunge wa Jimbo la Bumbuli kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mheshimiwa January Makamba ameandika ujumbe ambao kama kweli unaweza kufanyiwa kazi basi unaweza kuwainunua “milele” kiuchumi wasanii wetu wa filamu nchini na kuwawezesha kuondokana na hali ya vipato duni dhidi ya kazi zao kubwa wanazozifanya za uelimishaji wa jamii kupitia sanaa ya uigizaji na filamu.
Katika ujumbe huo Mheshimiwa makamba ametoa takwimu hizi kama ifuatavyo.
“There're 130 mil Swahili speakers. If only 1% buy a Bongo movie at Sh 5,000/=, that's Sh 6.5 billion. If an artist gets 20%, that's 1.3 bil”
Akimaanisha kuwa;-
Kuna karibu watu milioni mia moja na Thelathini (130 mil) wanaozungumza Kiswahili. Kama angalau asilimia moja ya watu hao milioni mia moja na thelathini – yaani watu milioni moja na laki tatu (1,300,000) wakinunua filamu hizo kwa shilingi elfu tano tuu kwa filamu moja, itapatikana shilingi bilioni sita na nusu (6.5 bil) toka kwenye mauzo hayo- na kama msanii atapata angalau asilimia ishirini (20%) ya mauzo hayo basi atajipatia shilingi bilioni moja pointi tatu (1.3 bil) - pesa ambazo kiukweli zitamkomboa kabisaaa kwenye umaskini.
Je, maoni haya anweza kuwa kweli? Kama ndiyo ni kitu gani kifanyike basi? Tupe maoni yako. 

Previous Post Next Post