Mourihno
Mourihno
Ronaldo akipunga mkono jambo ambalo limewashangaza na kuwastua mashabiki wa Madrid
Mourihno akimpa maelekezo Essien
KOCHA Jose Mourinho jana aliwaaga mashabiki wa Real Madrid katika mchezo wa mwisho wa La Liga alipokea kelele za kushangiliwa na kuzomewa wakati timu yake ikiifunga Osasuna 4-2 Uwanja wa Bernabeu.
Lakini kulitokea sintofahamu kuhusu mustakabali wa mchezaji anayewaniwa na Manchester United na Chelsea, Cristiano Ronaldo, ambaye aliikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi.
Kocha huyo Mreno alitoa taarifa fupi ya kuaga katika tovuti ya Madrid saa chache kabla ya mechi na Osasuna.
Baada ya mechi, Mourinho, ambaye anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kurejea Chelsea msimu ujao, aliwapungia mono mashabiki kuwaaga kabla ya kuondoka uwanjani.
Mourinho, ambaye katika maisha yake ya ukocha anajivunia kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa na ubingwa wa Ligi za Ureno, England, Italia na Hispania Spain anatarajiwa kurejea Chelsea msimu ujao.
Baada ya kushinda Kombe la Mfalme katika msimu wake wa kwanza na Ligi Kuu ya Hispania katika msimu wa pili, Mourinho na klabu zilikubaliana kuachana baada ya msimu huu wa tatu.
Mourinho amekuwa akishambuliwa mno kwa kumuweka benchi Nahodha na kipa Iker Casillas msimu huu na akionekana kuwapendelea baadhi ya wachezaji kama Pepe.
Wachezaji wengine wa Madrid wamemtakia kila la heri Mourinho.
Katika mchezo wa jana, Gonzalo Higuain aliifungia Madrid bao la kuongoza dakika ya 35, kabla ya Michael Essien kufunga la pili dakika nne baadaye.
Osasuna ilisawazisha kupitia kwa Roberto Torres na Alvaro Cejudo.
Karim Benzema akaisawazishia Real zikiwa zimesalia dakika 20 kabla ya bao la dakika za lala salama la Jose kuihakikishia ushindi Madrid.