Hii ni Kutoka Kwa Gosby atoa nafasi kwa wasichana 3 leo kwenda kusikiliza exclusively wimbo wake mpya BMS



Rapper wa B’Hits, Gosby ametoa nafasi kwa wasichana watatu wenye bahati watakaopata nafasi ya kwenda kusikiliza kwa mara ya kwanza wimbo wake mpya, Baby Making Swag aka BMS, unaotarajiwa kuachiwa Ijumaa hii.
BLP_lSVCQAAOv8P
Listening session hiyo itafanyika saa moja usiku Alhamis hii kwenye studio za B’Hits.
Gosby atatumia akaunti yake ya Twitter kuchuja wasichana hao na tayari ameshapata wasichana 18 wanaotaka kuwepo.
Ameiambia Bongo5 kuwa amechagua wasichana peke yake kuwepo kwenye session hiyo kwakuwa BMS inawahusu zaidi wao japo kuna kitu amekiandaa kwa wanaume pia.
“I think wasichana watakuwa wa kwanza kuipenda hii nyimbo that’s why nimeanza nao,”anasema.
Gosby amesema ameamua kufanya hivyo ili kuwafanya mashabiki wake kuwa wa kwanza kuusikiliza wimbo huo.
“Nilikaa nikafikiria kwamba nifanye kitu fulani kiwe special kwa mafans kwasababu kila siku watu wakiwa wanataka kutoa wimbo huwa wanawachukua baadhi ya watu peke yake ndio wanaenda kusikiliza nyimbo kabla haijatoka, mashabiki wanaopenda miziki yetu wanakuwa wapo nyuma, wanakuwa watu wa mwisho kusikiliza products ambazo sisi tumefanya.”

Huyu Hapa  zaidi

.
Previous Post Next Post

Popular Items