MULLA JUKWAA MOJA NA SNOOP




Wasanii wanaoliunda kundi maarufu la miondoko ya Hip Hop nchini Kenya, Camp Mulla wanaendelea kula mashavu na habari iliyopo ni kuwa wakaree hao wanatarajia kutumbuiza sambamba na nyota wa miondoko ya kufoka nchini Marekani Snoop Doggy Dogg ambaye hivi sasa amegeukia urasta na kujipachika jina la Snoop Lion.

Camp Mulla ambao hivi sasa wapo kimataifa zaidi kutokana na juhudi zao katika muziki watatumbuiza na nyota huyo katika tamasha moja la ‘Africa All Stars KwaZulu-Natal Concert’ ambalo litafanyika tarehe 18 ya mwezi huko Dublin ambapo pia wasanii mbalimbali barani Afrika wanatarajia kutoa shavu kwenye tamasha hilo wakiwemo Fally Ipupa, Professor, 2Face, Flavour, Zakes Bantwini, Zahara, D’Banj na Big Nuz wa nchini Kenya.

Hii ni nafasi nzuri zaidi kwa kundi hili la Camp Mulla haswa baada ya uvumi kutanda kuwa wametengana lakini jibu unalo we mtazamaji wa eNewz jamaa wanakata mawingu na kama ujuavyo hawazichezei nafasi hizo adimu katika tasnia nzima ya muziki na burudani.

Previous Post Next Post