MASTAA MAREKANI WASHTUSHWA NA SHAMBULIO LA BOSTON

meek-mill
Kufuatia milipuko miwili ya Jana huko Boston karibu na mstari wa kumalizia mbio ndefu za Boston ambapo watu watatu wameripotiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, watu maarufu mbalimbali wakiwemo mastaa wa muziki wa Hip Hop wameungana kwa kuwafariji majeruhi wa mlipuko huo.
Meek Mill ni kati ya watu ambao anasema alikuwa Boston saa chache tu kabla ya tukio hili kutokea na kuonyesha kushtushwa na habari hizi, French Montana pamoja na Chris Brown pia ni moja kati ya watu ambao wamesema kuwa sala zao wanazielekeza kwa watu wa Boston.
Gonga continue reading kuendelea..

Kelvin Hart pamoja na Spitta ni kati ya wengine wengi ambao wametumia mitandao ya jamii kuwafikishia mashabiki wao ujumbe wa hisia zao za huzuni kuhusiana na maafa ambayo yamewakumba wote walioathiriwa huko Boston.
Previous Post Next Post