JB APANGA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015


Mwigizaji anayependwa sana na mwenye mwili wa kipekee kwenye bongo movies Jacob Steven, ama JB kama anyofahamika kwa wapenzi wake, ameongea na bongomovies.com na kuelezea mpango wake wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015. Katika interview fupi iliyofanyika maeneo ya leaders jijini Dar es salaam leo, JB alisema angependa kuwakilisha wananchi kwani kupitia sanaa ameweza kujifunza matatizo mengi yaliyopo kwenye jamii na anahitaji nafasi ili ayafanyie kazi.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hii ni kwanini amepata wazo hilo saivi JB alisema kuwa amewahi kushiriki kwenye shughuli nyingi sana za kampeni kama “manager” wa kampeni za wabunge mbalimbali na kupata uzoefu wa siasa na pia karibu wote waliweza kupita kwenye nafasi hizo na sasa anaona ni wakati wake yeye kuwawakilisha wananchi bungeni.

Na alipoulizwa kuhusu suala la chama na sehemu anayopanga kuiwakilisha JB alisema, “kwa sasa siwezi kuweka wazi kuhusu chama na sehemu nayotaka kugombea ubunge, ila wapenzi wangu wakae tayari na wajue mipango yangu kama mwigizaji na mtu anayependa mandeleo kwa jamii”
Previous Post Next Post