MAMA BILAL ATOA TUZO SIKU YA MWANAMKE DUNIANI


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, . Picha na OMR.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya hundi ya Sh. milioni 6, mshindi wa kwanza wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume, wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na OMR).
 Picha juu na chini ni Washiriki wa onyesho la mitindo ya mavazi ya Mwanamakuka, wakipita jukwaani wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, ambapo zawadi hizo zilikabidhiwa na Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,  katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mama Asha Bilal, akishiriki pamoja na wageni waalikwa kuburudika kucheza muziki wa kizazi kipya wa Msanii Q-Chilla, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Mwanamakuka zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Mwanamke Duniani,  katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, na baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki kucheza muziki na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baby Husna, wakati akitoa burudani kwenye hafla ya kutoa tuzo za Mwanamakuka 2013 zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Wanawake Duniani, katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam 
Mke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wadhamini waliofanikisha kufanyika kwa hafla hiyo ya utoaji tuzi za Mwanamakuka 2013, baada ya kukabidhi tuzo hizo kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Previous Post Next Post

Popular Items