JE UNAJUA BAMBOO AMESEMA NINI KUHUSU BEEF YAKE NA PREZZO? SOMA HAPA ZAIDI



Bamboo.

Rapper Bamboo kutoka area 254 kwa Uhuru Kenyatta ameongea kwa mara ya kwanza kuhusu beef iliyokuwepo kati yake na rapper mwenzake wa Kenya AMB Prezzo, beef ambayo imekuwepo kwa kitambo huku pia chanzo kamili kikiwa hakifahamiki.

Kwenye interview na presenter wa Citizen Tv/Radio Mzazi William Tuva, Bamboo amesema “ilikua ni ushindani tu yani, wakati huo tulikua tunaona hiphop ni ya watu wa mtaa na sio wale matajiri lakini mwisho wa siku ni ushindani mzuri, tukapatana na tukajuana baada ya hapo tukaanza kuelewana na kuwa marafiki na kula goodtimes pamoja, hatuna beef tena na hata juzi alipoteza dem wake Goldie tukaenda kumpa pole bwana…. hivi karibuni kuna kazi zangu mimi na yeye zitakuja”


Prezzo.

Bamboo ni mmoja kati ya wasanii waliojitokeza waziwazi kumpa support mgombea kiti cha Urais Kenya Uhuru Kenyatta ambae alitangazwa mshindi baadae, baada ya hapo kumekua na stori nyingi kwamba Jaguar na Bamboo wameahidiwa kulipwa pesa nyingi kama mshahara wa kazi waliyofanya kwenye kampeni.

Bamboo amesema mpaka sasa hawajalipwa chochote, pamoja na kwamba anajua kina Uhuru Kenyatta ni matajiri.. wao kama wasanii walijitolea tu kufanya hiyo kazi baada ya kuguswa na moja kati ya sera za wagombea kuhusu kuwasaidia vijana wengi wa Kenya kwenye dunia ya sasa ya teknolojia
Previous Post Next Post