Mshindi wa nne wa DStv Rewards Bwana Edward Hiza Mhina (katikati) akipotea hundi ya shilingi milioni tano (5,000,000/=). Kulia ni Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi na Meneja wa Fedha wa kampuni hiyo, Francis Senguji. DStv inatoa kila wiki Tshs 5,000,000 kwa wateja wake ambao watalipia malipo ya mwezi ya akaunti zao za DStv kabla ya kukatika.
Wateja wa DStv ambao wanalipia malipo ya mwezi ya akaunti zao kabla ya kukatika wanaendelea kubahatika na kuibuka washindi wa mamilioni ya pesa kila wiki. Hiyo ni kupitia droo maalumu ya DStv ambayo imepewa jina la DStv Rewards.
Mteja ambaye amebahatika kuibuka na kitita cha Tshs Milioni 5 wiki hii na hivyo kuifanya idadi ya washindi kufikia wanne ni Bw. Edward Hiza Mhina, mkazi wa Dar-es-Salaam.
Bw. Mhina anasema yeye, kwa miaka nenda rudi, amekuwa mteja wa DStv. Familia yake imekuwa ikifurahia kwa pamoja vipindi mbalimbali vinavyorushwa kupitia DStv na hivyo DStv imekuwa sehemu ya familia yao.
Edward Hiza Mhina akiwa ameshikilia mfano wa hundi ya Tshs 5,000,000 ambazo amejishindia kupitia DStv Rewards.
Ameshukuru na kufurahia kuibuka mshindi kwani ni wazi kwamba ni kitu ambacho hakukitegemea. Nilipomuuliza atazitumia vipi fedha alizozipata, Bw. Mhina alisema “Nitajadiliana na familia yangu jinsi ya kuzitumia lakini ninachojua ni kwamba kiasi fulani kitatumika kwenye kuendelea kulipia DStv na zingine tutazitoa kwenye shirika au mashirika yasiyo ya kiserikali kutegemea uamuzi wa familia”
WAKATI HUO HUO: Mteja wa DStv, Togani Ngotta,ameibuka mshindi katika droo nyingine ambayo imepewa jina la Spot The Rewards Box ambapo pindi mteja akiwa anatizama televisheni na kufanikiwa kuona kibox fulani chenye nembo ya DStv, anatakiwa kutuma SMS yenye majina yake yote mawili na namba yake ya simu kwenda katika namba +27 711 745 622 ndani ya dakika tano tangu alipokiona “kibox”.
Kwa ushindi huo Togani Ngotta ameshinda Subscription ya mwaka mzima (miezi 12) ya DStv.Kwa maana hiyo, Bw.John ataendelea kufaidi DStv bila malipo yoyote kwa kipindi cha mwaka mzima!
Mshindi wa Shindano la Spot The Rewards Box, Togani Ngotta (katikati) akipongezwa na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kulia).Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu.