Wachimbaji wa madini wamekuwa wakitumia raslimali nyingi kama vile fedha, nguvu kazi na mashine ili kuweza kuchimba ardhi, kuvunja miamba na kupembua mchanga na udongo ili kupata madini ya dhahabu kwenye maeneo ya machimbo.
Kwa mfano hapa nchini Serikali imekuwa ikitoa msamaha wa mabilioni ya kodi mbalimbali kila mwaka kwa kigezo cha wawekezaji kutumia fedha nyingi katika kufanikisha upatikanaji wa madini.
Kutokana na kigezo hicho cha msamaha wa kodi pamoja na mapato kidogo yanayokusanywa na serikali kwenye sekta ya madini ukilinganisha na fedha nyingi za mauzo, imekuwa ikiwakatisha tamaa Watanzania wengi kiasi cha kutaka mikataba ivunjwe.
Watanzania wengi wanaamini kwamba madini mengi yanayochimbwa na wawekezaji yanawafaidisha tu wawekezaji na kuwaacha wananchi wakiendelea kuogelea kwenye dimbwi la umaskini.

Dhahabu hupatikana hapa nchini na ni moja ya madini yenye thamani kubwa duniani na bidhaa zote zinazotokana nayo, huuzwa kwa bei kubwa.
Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha McMaster kilichopo nchini Canada wamekuja na ugunduzi ambao unatoa picha kwamba huenda madini ya dhahabu yakatengenezwa maabara na kuachana na mtindo wa kutumia fedha nyingi kuyachimba ardhini.

Wazo hilo linakuja baada ya watafiti hao kubaini kuwa kuna bakteria wenye uwezo wa kutengeneza dhahabu wanapukuwa katika mazingira fulani.
Wanasayansi hao wamenukuliwa na Jarida la Nature Chemical Biology, ambalo hupatikana pia kwenye mtandao wa kompyuta, wakielezea mfumo mzima wa jinsi bakteria hao wanavyotengeneza dhahabu.Utengenezaji dhahabuBakteria ni moja ya kundi la viumbe hai ambalo jamii yake imegawanyika kwenye makundi mengi pengine kuliko viumbe wengine.Kutokana na bakteria kuwa wa aina nyingi ndiyo maana ndio kundi linalosababisha magonjwa ya aina mbalimbali kwa binadamu.
Vile vile, wapo bakteria wazuri na wenye faida kwa binadamu ambao humsaidia katika mambo mbalimbali kwa mfano wale wanaokaa kwenye mfumo wa chakula ambao humsaidia katika umeng’enyaji.
Aina ya bakteria ambayo wanasayansi wamegundua kuwa na uwezo wa kutengeneza dhahabu wanajulikana kwa jina la kitaalamu la Delftia acidovorans.Namna anavyotengeneza dhahabuWakitafiti jinsi bakteria hao wanavyotengeneza dhahabu, wanasema hufanya hivyo wakati wakijijengea kinga dhidi ya sumu inayoweza kuwadhuru kutoka kwenye mfumo wa kikemia.
Katika sayansi rahisi ni kwamba bakteria hao huunda dhahabu wakati wanapokumbana na mfumo wa kemikali zinapokutana kusababisha aina mpya ya kemikali.
Katika sayansi rahisi ni kwamba bakteria hao huunda dhahabu wakati wanapokumbana na mfumo wa kemikali zinapokutana kusababisha aina mpya ya kemikali.
Mfano asidi inapokutana na alkali zao lake ni kupata chumvi na maji. Lakini wakati Alkali na Basi zinakutana kuna mchambuo wa kuvunjikavunjika kwa vile vitu vilivyounda kemikali hizo ili zifanye maongano mapya yatakayosababisha mazao ya kemikali nyingine.
Vile vitu vilivyovunjika kwenye mchambuo huo huitwa atomu. Atomu hizo kisayansi zinakuwa zimepoteza elektroni hivyo hutafuta mwenzi wa kuungana naye.
Atomu zilizoko kwenye harakati za kutafuta mwenza wa kuungana naye ndizo ambazo ni adui mkubwa wa bakteria aina ya Delftia acidovorans, hivyo hujiwekea kinga.
Atomu zilizoko kwenye harakati za kutafuta mwenza wa kuungana naye ndizo ambazo ni adui mkubwa wa bakteria aina ya Delftia acidovorans, hivyo hujiwekea kinga.
Katika kujiweka kinga hiyo, bakteria hawa hutoa kemikali ambayo huifanya ijifunike pande zote asidhurike na atomu hizo.
Kemikali hiyo ya ulinzi kwa bakteria hutokana na aina ya protini inayotolewa na bakteria huyo ijulikanayo kama delftibactin A.
Kemikali hiyo ya ulinzi kwa bakteria hutokana na aina ya protini inayotolewa na bakteria huyo ijulikanayo kama delftibactin A.
Katika harakati hizo, bakteria hao hujikuta wakifanya kazi ya kufanya atomu hizo ziwe za kutengeneza dhahabu ambayo kwake haina sumu ya kumdhuru.
“Huu ni ugunduzi ambao unaweza kuweka mfumo wa kisayansi wa kutengeneza dhahabu,” anasema Kiongozi wa Timu iliyofanya utafiti huo, Profesa Nathan Magarvey wa Chuo Kikuu cha McMaster kilichopo katika mji wa Hamilton, jimbo la Ontario, nchini Canada.
Profesa Magarvey anasema ugunduzi wao pia unaweza kusaidia kuunda mashine ambazo zinaweza kubaini maeneo ambayo yana utajiri wa madini ya dhahabu.Kwa maoni, maswali wasiliana nasi kwa simu: 0713 247889 au baruapepe: ulimwenguwasayansi@ymail.com
Chanzo:Mwananchi