Kwa mujibu wa utafiti wa Daktari Brizendine, tofauti na mwanammke, tangu umri wa kubalehe, ubongo wa mwanamme umeumbwa ukiwa na nafasi kubwa yenye kuweza kusajili hofu. Unapeleka nguvu za kushambulia pia, kutumia misuli zaidi. Wenye kumpelekea mwanamme kuwa na hulka za kujilinda na zaidi kulinda eneo lake la miliki, hata kwenye mahusiano. Homoni hizi huchochea nguvu za kushambulia kwa madhumuni ya kujihami.
Ni katika hali hii, ndipo baadhi ya wanaume huwa tayari kufa kuwapigania wapenzi wao.
Swali ni hili, je, kuna utafiti, ama uzoefu wenye kuonyesha kuwa mwanamke naye kwenye ubongo wake anazo homoni na misuli yenye kumfanya aweze kuwa tayari kufa kumpigania mpenzi wake? Maana, tumeona pia, katika maisha, wanawake waliojitoa muhanga kwa ajili ya wapendwa wao.
Bongo 61 tunakaribisha maoni yenu...