TIGO YAMWEZESHA MSHINDI WA DROO YA SMART CARD ' LIVE' MECHI KATI YA REAL MADRID NA FC BARCELONA NCHINI HISPANIA.


Meneja wa Tigo Bw. William Mpinga akimkabidhi Bw.Julius Raphael Kanza ambaye ni mshindi wa Smartcard droo mfano wa tiketi ya kwenda kushuhudia pambano la ligi kuu Uhispania kati ya Real Madrid na Fc Barcelona mwezi March mwaka huu.

Kampuni ya Tigo leo imemkabidhi mshindi wa smartcard droo Bw. Julius Raphael Kanza Tiketi ya kwenda nchini Hispania kushuhudia pambano la ligi ya uhispania La Liga kati ya Real Madrid na Fc Barcelona mwezi Machi.

 Makabidhiano hayo yalifanywa na Meneja wa chapa Tigo Bw.William Mpinga leo kwenye ofisi za Tigo ikiwa ni usafiri wa kwenda na kurudi, malazi na chakula vyote bure.

 Akizungumza Bw. Kanza amesema hakutegemea kupata fursa hiyo na ilikuwa kama ndoto, kwanza alidhani ni utapeli kumbe si hivyo, na amewashukuru sana Tigo kwa kumuwezesha na amewashauri watumiaji waTigo wajiunge na huduma ya smartcard nao wabahatike.

Hizi ni droo za kila mwezi ambazo washindi wa zawadi tofauti hupatikana na droo kubwa ndio inamtoa mshindi wa mwaka.

Previous Post Next Post