TAMASHA LA MSIMU WA "TABASAMU UPO NA TIGO" LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM - COCO BEACH



Pichani Juu na Chini ni Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka TMK  Mh Temba sambamba na Chege wakimwaga mistari wakati wa uzinduzi wa msimu wa Tabasamu ambao umetokana na Tigo kubadilisha kauli mbiu yake ya zamani kutoka “Jielezee mwenyewe” kuwa “Tabasamu! upo na Tigo” uliofanyika katika fukwe za Coco Beach jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa mtandao wa Tigo.


Niepnde kama nilivyo…..si mwingine ni Mr. Blue a.k.a Kabaisa akiwapa raha wakazi wa jiji la Dar waliofurika kwenye fukwe za Coco Beach kushuhudia uzinduzi wa tamasha la “Tabasamu! upo na Tigo”.

Msanii nyota wa muziki wa Hip Hop nchini ROMA akichana mistari mbele ya umati wa maelfu ya wakazi wa jijini Dar  katika fukwe za Coco Beach ambapo kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imezindua kauli mbiu yake mpya iitwayo “Tabasamu! upo na Tigo”. Tamasha hilo limeratibiwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd.

ROMA akiimba sambamba na mashabiki wake.

Msanii wa kizazi kipya uzao wa THT, anayefahamika kwa jina la Rachel akitumbuiza maelfu ya watu waliofika kushuhudia uzinduzi wa msimu wa Tabasamu ambao umetokana na Tigo kubadilisha kauli mbiu yake ya zamani kutoka “Jielezee mwenyewe” kuwa “Tabasamu! upo na Tigo”.

Previous Post Next Post