TAARIFA KUHUSU KANISA LILILOCHOMWA MOTO ZANZIBAR USIKU WA KUAMKIA JANA FEB 19.

Hii ni picha ya liblary lakini ni moja ya Makanisa yaliyowahi kuchomwa Zanzibar.


Ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuuwawa kwa risasi kwa padre Evarist Mushi huko Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadae kulichoma moto kanisa la Walokole la Shaloom lililoko Kiyanga kwa Sheha mkoa wa kusini Unguja Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoa wa kusini Unguja Agustino Ulomi amesema hilo tukio limetokea jana saa tisa na nusu usiku, ambapo huo moto ulianza kuwaka baada ya vijana watatu walioonekana karibu na kanisa, baadae kidogo ndio mlinzi akaanza kusikia mawe yakirushwa juu ya bati.
Baada ya mlinzi kuona hatari ilibidi akajifiche lakini kwa mbali akawa anaona kinachoendelea, moto ukiendelea ndio akampigia simu kiongozi wa kanisa ambae aliwapigia polisi, wakaja wakawa wanashirikiana na wananchi kuuzima japo tayari ulikua umeshaunguza samani mbalimbali za kanisa hilo, kilichosaidia kanisa hilo kutoungua lote ni vifaa imara vilivyotumika kulijenga.
Katika ripoti hii ambayo imeripotiwa na mwandishi wa habari Cathbert Kajuna wa kajunason.blogspot.com bado hajakamatwa mtu yeyote mpaka sasa, polisi wamesema pia wanaanza utaratibu wa ulinzi wa makanisa kutokana na vitisho vilivyopo sasa hivi.
Nimeongea na mwandishi wa habari wa millardayo.com kutoka Zanzibar jioni hii, kasema hakuna mtu yeyote aliejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea saa tisa usiku wa kuamikia leoendelea kuwa karibu na Bong61.com facebook.com/bongo61 kwa ajili ya update muhimu!!
Previous Post Next Post