RWANDA YAJIIMARISHA KUKABILIANA NA MAAMBUKIZI YA VVU KATIKA MAENEO YA MJI WA KIGALI.


Jiji la Kigali kwa sasa limeweka kipaumbele katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuwa kiwango cha maambukizi katika mji huo ni kikubwa kuliko maeneo ya pembezoni.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya ya Jamii nchini humo Dkt. Blaise Uhagaze amesema kiwango cha maambukizi katika mji wa Kigali ni asilimia 7.3, ambacho ni sawa na mara tatu zaidi ya maeneo ya vijijini, huku kiwango cha maambukizi kitaifa kikiwa ni asilimia 3.

Amesema pamoja na mambo mengine lakini kiwango cha watu kukimbilia mjini na kuwepo kwa makazi ya watu wengi ni moja wapo ya sababu za kuongezeka kiwango cha maambukizi mjini kuliko vijijini.

 

Previous Post Next Post