MWAI KIBAKI ATEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA



 Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magareza nchini, Kamishna Jenerali John Minja kabla ya kuingia ndani ya  Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, anayefuata ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.

Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (wapili kutoka kulia) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kushoto),  Mkuu wa Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na maofisa mbalimbali kutoka nchini na Kenya, wakiingia ndani ya kiwanda hicho.
Mshauri Mtaalamu wa Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu katika Jeshi la Magereza, Alpherio Moris (kulia) akimuonyesha Rais Mwai Kibaki moja ya kofia ngumu (Helmet) ambayo inatarajiwa kutengenezwa na kiwanda cha magereza Ukonga hivi karibuni.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jeneral John Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum ya kiti Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Rais Mwai Kibaki (wa kwanza kutoka kulia aliyevaa tai) akiwafurahia Askari Magereza na ofisa kutoka nchini Kenya wakiwa wamekaa kwenye kiti cha wapendanao kilichotengenezwa na wafungwa kiwandani humo.
 Rais Mwai Kibaki (wa pili kushoto) akiwa na maofisa mbalimbali wakiondoka Kiwanda cha Magereza Ukonga baada ya kumaliza kuangalia vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.

Previous Post Next Post