Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha orodha ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013 hospitalini hapo. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani na vina thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha moja ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013. Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine za Ulta Sound, X-Ray, Upasuaji, tiba ya macho, tiba ya kinywa na meno, mgongo, mifupa, mashine ya dawa za usingizi, vitanda maalum (TCU beds) n.k. Kushoto anaeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Baadhi ya vifaa tiba alivyokabidhi Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia saba. Vifaa hivo pamoja na vingine ambavyo bado vipo kwenye kontena vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani.
Mama Salma Kikwete akiongea na wadau wa sekta ya afya na wananchi waliokusanyika katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkaribisha Mama Salma Kikwete kuzungumza na wadau wa afya katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ambapo alikabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Mama Salma kwa jitihada anazozifanya yeye na taasisi yake katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha huduma za afya nchini, alimuhakikishia kuwa Serikali yake ya Mkoa itahakikisha inasimamia vizuri sekta ya afya kutimiza ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2010-2015 ambazo ni pamoja na kuimarisha huduma za afya nchini.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daudi Nasib akielezea kwa kifupi kazi na majukumu ya taasisi hiyo kwa wadau wa afya waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka WAMA kwa uongozi wa hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa. Miongoni mwa malengo makuu ya taasisi hiyo ni kuimarisha afya ya mama na mtoto na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini.
Ndugu Abdul Kimario wa shirika la Project C.U.R.E kutoka Marekani ambae shirika lake limeshirikiana na WAMA kuleta vifaa tiba hivyo hapa nchini akitoa ufafanuzi wa matumizi ya baadhi ya vifaa hivyo kwa wadau wa afya waliokusanyika kushuhudia makabidhiano hayo.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mzee Protas Kimario kitambulisho cha matibabu ya uzeeni kuwakilisha wazee wengine 458 zoezi lililoenda sambamba na kukabidhi vifaa vya tiba kwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.02.2013. Jumla ya vitambulisho 4356 sawa na asilimia 96% katika Manispaa ya Sumbawanga vimeshatengenezwa kwa ajili ya matibabu ya wazee.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta funguo za pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya vya Wilaya hiyo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Jumla ya Pikipiki kumi kutoka Water Rid zilikabidhiwa kwa ajili ya huduma hizo katika Mikoa ya Rukwa na Katavi.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)