DW KUADHIMISHA MIAKA 50 IDHAA YA KISWAHILI


images
Deutsche Welle inaadhimisha miaka 50 ya idhaa yake ya Kiswahili
chini ya maudhui ya “Maarifa na Mwamko“ katika hafla maalumu
itakayofanyika jijini Dar es Salaam
Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari
za uhakika kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya
Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu. Tarehe 22 Februari, saa
9.oo mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa, DW itasherehekea
maadhimisho haya kwa hafla maalumu jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwa-
leta pamoja wachambuzi wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui ya
“ Maarifa na Mwamko kupitia Vyombo vya Habari“.

Hotuba maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa
Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya
Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt.
“Idadi kubwa ya wasikilizaji wetu wanaishi hapa Tanzania, kwa hivyo
lilikuwa chaguo la uhakika kwa ajili ya sherehe zetu,“ alisema Andrea
Schmidt. “Kwa miaka 50 iliyopita, DW imejitolea katika utoaji wa habari
zenye uwiano na taarifa za uhakika, ikiwapa watu wa Afrika ya Mashariki
habari na uchambuzi wa kina juu ya masuala yenye uzito mkubwa.“
Uchambuzi utafanywa na jopo la majadiliano lililotayarishwa kwa msaada
wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ofisi ya Dar es Salaam na
utafanywa kwa lugha ya Kiswahili. Mohammed Khelef wa DW ataongoza
majadiliano hayo akiwa na wataalamu wa vyombo vya habari wanaoheshi-
mika nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew Mwambene (Mkurugenzi
Februari 2013


wa Idara ya Habari, Maelezo), Mohamed Abdulrahman (DW), Jenerali
Ulimwengu (Mwandishi wa habari), Valerie Msoka (Mkurugenzi wa
TAMWA) na Maggid Mjengwa (Mtaalamu wa mitandao ya kijamii).
Wahudhuriaji watakuwa pia na fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo
na waandishi wa DW kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania, ambao wanahudhuria hafla hiyo katika
jengo la Makumbusho ya Taifa
Previous Post Next Post