NA Maelezo ZanzÃbar
Mjumbe wa Baraza kuu la Ungozi la Chama cha Wananchi CUF Juma Duni Haji amewataka Wazanzibari kuongeza mshikamano na kujiepusha na itikadi za vyama vyao katika kutetea maslahi ya ZanzÃbar kwenye Muungano.
Juma Duni ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wafuasi wa CUF katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiwanja cha Komba wapya Mjini ZanzÃbar.
Amesema njia pekee ambayo itawasaidia kupata maslahi wanayoyataka katika Muungano ni kuwepo kwa umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari jambo ambalo ni chachu ya mafanikio.
Ameongeza kuwa kwa muda mrefu ZanzÃbar imekuwa ikibanwa na mambo mengi yanayohusu uchumi wake katika Muungano na kwamba sasa ni muda muafaka wa kupigania Muungano ambao utakuwa wa haki na usawa baina ya ZanzÃbar na Tanganyika.
Juma Duni ambaye pia ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ZanzÃbar amewataka Wazanzibari kuendeleza kudumisha amani iliyopo ZanzÃbar sambamba na kutii sheria zilizopo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza Kuu CUF Ismail Jusa Ladu amedai kuwa Wazanzibari wanachotaka katika Katiba mpya ni Muungano ambao utatoa haki sawa baina ya ZanzÃbar na Tanganyika.
Amedai kuwa Mshikamano ambao waliuonesha Wazanzibari katika kutoa maoni umewajengea uwezo watu wengine kutoka Bara kuwaunga mkono katika kutetea Muungano ambao unaipa hadhi ZanzÃbar.
Mkutano huo umekuja ikiwa ni mwendelezo wa kuhamasisha uhai wa Chamana kutoa elimu ya Muungano kwa wanachama wa chama hicho.
elimu ya Muungano kwa wanachama wa chama hicho