DAR YAONGOZA KURA ZA TAMASHA LA PASAKA



WAKAZI wa jijini Dar es Salaam wamepongeza mkoa wao kuwa wa kwanza kuchaguliwa kupata nafasi ya kuandaa tamasha la Pasaka  mwaka huu kwa sababu limezingatia matakwa ya mashabiki ya tamasha hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema mfumo wa upigaji kura kwa njia ya sms unaofanyika kwa sasa unasaidia wadau kupigia kura mikoa yao

.
Eunice Muhandia alisema inaonyesha Dar es Salaam kuwa na wakazi wengi hali ambayo imesababisha kupata nafasi ya kwanza, ingawa hata Mwanza na Arusha kuna idadi ya wakazi inayokaribiana na Dar es Salaam, hivyo mikoa mingine iongeze kasi ya upigaji kura ili wapate fursa ya kuandaa tamasha hilo.
Muhandia alisema kwa mfumo ulioanza mwaka huu, utaliimarisha zaidi kutokana na kuwashirikisha wadau ambao ndio wenye tamasha lao.
Naye Janeth Christopher ambaye ni muimbaji wa injili chipukizi alisema fursa ya kuwapata waimbaji watakaoshiriki itawasaidia kwa sababu walikuwa hawana namna ya kuweza kupata nafasi ya kushiriki.
Janeth alisema awali walidhani kwamba, tamasha linaendeshwa kwa mfumo wa mtu mmoja ambaye ni Alex Msama kumbe linatushirikisha hata sisi wadau, jambo ambalo anaipongeza kamati ya maandalizi kwa kuwaona.
Aidha wakati taratibu za maandalizi ya tamasha hilo zikiendelea, wadau wanatakiwa kupiga kura katika mikoa yao ili kukamilisha mikoa takribani  saba ambayo inategemewa kufikiwa na tamasha hilo, wadau wanatakiwa kupiga kura kwa kuandika neno gospo halafu jina la mkoa unaotaka lifanyike na utume kupitia namba 15522.    
Wakati zoezi hilo likifanyika, litakalofuata ni zoezi la kuwapata waimbaji washiriki  ambao nao watapatikana kwa kuandika neono gospo, jina la mwimbaji, kikundi au kwaya na kuituma kwendanamba 15678.
Previous Post Next Post

Popular Items

Kenya katika hatari ya kupata Ebola

Picha: Soggy Doggy Aongeza Familia