Kundi D kesho linakamilisha mzunguko wa pili kwa timu 16 zinazowania taji la ubingwa wa Kombe la Afrika barani Afrika kwa mwaka 2013.
 |
| Nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba |
Kivumbi kinatimuka kwa Ivory Coast kuanza kuonyeshana kazi na Tunisia katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo na kufuatiwa baadaye na Algeria itakayokuwa ikipambana na Togo.
Mpaka sasa Ivory Coast na Tunisia ndizo zinazoongoza kundi hilo zikiwa na pointi tatu kila moja baada ya kushinda michezo yao ya awali. Ivory Coast iliicharaza Togo huku Tunisia ikiibwaga Algeria.
Mchezo kati ya Algeria na Togo utakuwa wa ushindani zaidi huku kila timu ikitaka kushinda au kupata pointi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya robo fainali.
Tunisia ina kikosi imara kitakachopigana kuwaangusha miamba hao wa soka barani Afrika.
Tunisia imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika fainali za Kombe la Afrika, Lakini wamefanikiwa mara moja tu kutwaa kombe hilo ilipoandaa michuano hiyo mwaka 2004.
Wamekuwa katika fainali hizo tangu mwaka1994, ikiwa ni nchi pekee ya Afrika kufanya hivyo, lakini huenda walitarajia kupata mafanikio zaidi kutokana na wachezaji iliokuwa nao wakati wote huo.
 |
| Wachezaji wa Tunisia |
Kocha wa Tunisia Sami Trabelsi ni kipenzi cha mashabiki nchini Tunisia akiwa mchezaji maarufu wa sehemu ya ulinzi katika timu ya taifa, akishiriki katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka1996 na 2000, pamoja na zile za mwaka 1998 nchini Ufaransa.
Ivory Coast inajivunia nyota wake kadhaa wanaosakata kabumbu ndani na nje ya nchi hiyo.
Miongoni mwao ni Didier Drogba anayechezea nchini Uchina, Yahya Toure, mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2013 na pia tegemeo la timu ya Manchester City ya England, Wengine pamoja na timu wanazochezea kwenye mabano:
Walinda mlango:
Boubacar Barry (Lokeren, Ubelgiji), Badra Ali Sangare (IAFC), Daniel Yeboah (Dijon, Ufaransa).
Walinzi:
Soulemanye Bamba (Trabzonspor, Uturuki), Arthur Boka (VfB Stuttgart, Ujerumani), Emmanuel Eboue (Galatasaray, Uturuki), Igor Lolo (Kuban Krasnodar, Urusi), Siaka Tiene (Paris St Germain, Ufaransa), Kolo Toure (Manchester City, England), Ismael Traore (Stade Brest, Ufaransa)
Walinzi wa kati:
Max Gradel (St Etienne, Ufaransa), Abdul Razak (Manchester City, England), Romaric (Real Zaragoza, Hispania), Didier Ya Konan (Hannover 96, Ujerumani), Cheick Tiote (Newcastle United, England), Yaya Toure (Manchester City, England), Didier Zokora (Trabzonspor, Uturuki).
Washambuliaji:
Wilfried Bony (Vitesse Arnhem, Uholanzi), Didier Drogba (Shanghai Shenhua, China), Gervinho (Arsenal, England), Salomon Kalou (OSC Lille, Ufaransa), Arouna Kone (Wigan Athletic, England), Lacina Traore (Anzhi Makhachkala, Urusi).