Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Raymond Tshibanda. 
Kundi la waasi la M23 katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC limekubali kurejea katika meza ya mazungumzo na serikali ya nchi hiyo inayiwatuhumu kwa kuhusika na kufanya vitendo vyanavyo kwenda kinyume na haki za binadamu. 
Hayo yamewekwa wazi wakati ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC kupatiwa fursa ya kujibu tuhuma dhidi yake zilizotolewa na waasi hao kuhusu uongozi wa rais Joseph Kabila mwanzoni mwa mkutano huo.
Hapo awali ujumbe wa serikali ya Kongo ulimtaka Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Raymond Tshibanda kujibu tuhuma hizo, lakini wawakilishi wa waasi hao hawakutokea katika meza ya mazungumzo nchini Uganda.