Kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya kati, Florent Kyombo akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha)  ya kukamatwa kwa bidhaa zilizokwisha muda wake na zile zilizopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.Bidhaa hizo za zaidi ya tani tano na thamani ya zaidi ya shilingi 16 zimeteketezwa kwa moto.
 
 Kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya kati,Florent Kyombo (wa mbele) akikagua zoezi la kuteketeza bidhaa zilizokwisha muda wake na zile zilizopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu muda mfupi kabla hazijateketezwa kwa moto.
 
Mmoja wa vibarua waliopewa kazi ya kuteketeza bidhaa zilizopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu na zilizokwisha muda wake akizimwaga ili ziweze kuchomwa moto. (Picha na  Nathaniel Limu).
Na Gasper Andrew.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA) imeteketeza kwa moto tani tano za  bidhaa mbalimbali  ikiwemo vipodozi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.5 ambazo zimepigwa marufuku na zingine zilizomalizika muda wake.
Kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati Florent Kyombo, ameisema kuwa bidhaa hizo wamezikamawa wakati wa zoezi linaloendea mjini Singida kusaka bidhaa zilizopigwa marufuku na zile ambazo muda wake wa kutumika umeisha.
Kyombo amesema, bidhaa hizo zilikamatwa na maafisa wa mamlaka hiyo, kanda ya kati, wakishirikiana na wenzao wa manispaa Singida.
Akifafanua zaidi, amesema, katika msako huo  vipodozi na vyakula visivyoruhusiwa kwa matumizi ya binadamu vilikamatwa.
Kaimu meneja huyo amesema wamiliki wa maduka hivi sasa wanajitahidi kufuata sheria za TFDA, bidhaa ikimaliza muda wanaziondoa sehemu ya kuuzia na kuzitunza kwenye chumba maalumu, tayari kwa ajili ya maafisa wa TFDA kukagua na kuteketezwa.
Amesema baada ya kumaliza operesheni hiyo mkoani Singida mjini ambayo bado inaendelea, wataelekeza kampeni  katika wilayani Iramba.