![]() |
Rais wa marekani Barack Obama ameahidi kutumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa mkasa wa ufyatuliaji risasi kama ule uliotokea katika mji wa Newtown, jimbo la Connecticut, ambapo mtu aliyejihami kwa bunduki aliwauwa watu 26 wakiwemo watoto ishirini wa shule ya msingi hautokei tena. Akiwahutubia waumini wa madhehebu mbali mbali waliokesha kuwaenzi waliouwawa, bwana Obama alisema ili kuepuka mikasa kama hiyo, Marekani ni sharti ibadilike. BofyaRais Obama aliwaambia wakaazi wa eneo hilo kuwa taifa la Marekani linaomboleza. Watoto 20 na wanawake 6 waliuawa kwenye shambulio hilo lililotekelezwa katika shule ya Sandy Hook, na mtu mmoja ambaye pia alijiua kwa kujipiga risasi. |

Raia Connecticut wakiomboleza
Rais Obama kushinikza sheria mpya
Mazishi wa watoto wawili waliouawa kwenye tukio hilo yamefanyika hii leo.
Polisi wanasema mtu huyo aliyekuwa amejihami kwa bunduki na Adam Lanza mwenye umri wa miaka 20.
Mtu huyo alimuua mamake kwa kumpiga risasi kabla ya kuelekea shuleni anakofunza akiwa na gari lake.
Polisi wanasema mshukiwa huyo alikuwa na mamia ya risasi na alitumia bastola ya rashasha kama silaha yake maalum.
Mshukiwa huyo pia alikuwa amebeba bunduki zingine mbili ambazo zilipatikana ndani ya gari lake.
Kwa mara nyingine tena rais Obama alikariri haja ya kuchukua hatua dhidi ya uhalifu unaotekelezwa kwa kutumia bunduki, na kusema kuwa katika siku za hivi karibuni, atatumia kila mbinu na madaraka aliyo nayo kuhakikisha kuwa tukio kama hilo halitatokea tena.
Tags:
Uncategolized
