Afisa Utafiti Mwandamizi wa TRA Ephraim Mdee akielezea kuanza kwa mikakati ya urasimishaji wa tasnia za filamu na muziki na kuwasihi watanzania kuhakikisha wanashiriki katika kulinda, kuthamini na kuendeleza tasnia za filamu na muziki kwa kununua bidhaa zilizowekwa stempu za kodi. Katikati ni Katibu mtendaji Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo na kulia ni Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA.