
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, akisisitiza jambo kwa uongozi wa Mkoa wa Mwanza, Wakati treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL), ilipowasili Katika Stesheni ya Mwanza leo Mchana. Treni hiyo ilifanya safari yake ya Mwisho Mwaka 2009.Naibu huyo aliiipokea treni hiyo kwa kupanda kuanzia katika stesheni ya Malampaka mpaka Stesheni ya Mwanza. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bw. Baraka Kwanisaga. Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ni Mtahiki Meya wa Jiji La Mwanza Stanslaus Mabula(aliyevaa Flana Nyeupe).

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, akisisitiza wafanya biashara waliojenga vibanda na kufanyia biashara karibu na Miundombinu ya Reli katika eneo la stesheni ya Reli Mwanza mpaka Maeneo ya Mamlaka ya Bandari(TPA),kuhama katika maeneo hayo kama Sheria ya Reli inavyoelekeza.

Baadhi ya abiria wa wanaotumia usafiri wa Treni ya Shirika la reli Tanzania (TRL), waliotokea jijini Dar es Salaam ijumaa kuelekea Mkoani Mwanza wakiwa ndani ya behewa la Daraja la Tatu kama walivyokutwa leo asubuhi .Treni hiyo imeanza safari zake kutokea Dar kwenda Mwanza.


Wananchi wa Mwanza wakiipokea treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL), kwa ujumbe wa Mabango wakatii treni hiyo ilipowasili Mkoani Hap oleo mchana. Treni hiyo ilisitisha huduma zake tangu Mwaka 2009, Imeanza safari zake rasmi kwa mabehewa Sita, likiwemo moja la daraja la Kwanza. Treni hiyo itakuwa ikifanya safari zake Mara mbili kwa Wiki.
Tags:
Social