Mapema mwaka huu wamiliki wa kampuni  ya Anglo American walielezea kutofurahishwa na kudorora kwa faida za kampuni na kumtaka mwenyekiti kumwajiri afisa mkuu mtendaji mpya. Na hivyo kumtaka afisa mkuu wasasa  Cynthia Carroll kujiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita.
Lakini kampuni haijatangaza tarehe rasmi ya kuacha kazi kwa Cynthia. Hisa za kampuni hiyo zilipanda juu kwa asilimia mbili katika soko la hisa la London, lakini baadaye thamani ya hisa zake ilishuka kwa miezi minane iliyopita.
Cynthia alikabiliwa na shinikizo kutoka kwa wamiliki wa kampuni hiyo baada ya kampuni yake nchini Afrika Kusini kukumbwa na migomo katika mgodi wake wa Platinum wafanyakazi wakitaka kulipwa mishahara mizuri na kuwepo mazingira bora ya kazi